Loading

COVID-19 Vaccine Confidence Social Media Toolkit in Kiswahili

COVID-19 Vaccine Confidence

UJUMBE WA MITANDAO YA KIJAMII WA KUHIMIZA KUPATA CHANJO YA COVID-19

After the rapid development of the COVID-19 vaccines and subsequent rollout, there has been an infodemic of misinformation circulating about COVID-19 vaccine safety and efficacy, reducing public trust in getting vaccinated. This social media toolkit aims to support MOH officials, frontline health workers, community leaders and members, and patient advocacy groups with key messages to help address COVID-19 vaccine hesitancy in their communities.

This toolkit is also available in Nigerian Pidgin English, Luganda, and English.

Hashtags

#Vaccines Work #GetVaccines #VaccinesSaveLives #COVID19

#PataChonjoKE #PataChonjoKaaChonjo

Social Media Messages

Kulinda Jamii (na Kujilinda)

Hatua ya kuchanjwa italinda familia na marafiki zako kutokana na ugonjwa wa COVID-19. Wasiliana na kituo cha afya kilicho karibu nawe au angalia programu/tovuti ya Wizara ya Afya ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kupata chanjo ya COVID-19.

Hatua ya kuchanjwa italinda familia na marafiki zako kutokana na ugonjwa wa COVID-19. Wasiliana na kituo cha afya kilicho karibu nawe au angalia programu/tovuti ya National Primary Health Care Development Agency (NPHCDA) ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kupata chanjo ya COVID-19

Jamii na familia yako inakuhitaji. Pata chanjo yako leo au pindi inapopatikana katika kituo cha afya kilicho karibu nawe.

Ugonjwa wa COVID-19 unaweza kuwa na madhara ya kutishia maisha au ya kudumu. Pata chanjo ya COVID-19 sasa ili kujilinda wewe na familia yako.

Kupata chanjo dhidi ya COVID-19 kunaokoa maisha.

Tujenge upya jamii yetu ili iwe thabiti kuliko hapo awali. Pata chanjo ya COVID-19 haraka iwezekanavyo.

Pata chanjo ya COVID-19 sasa na usaidie kulinda familia, marafiki na jamii yako.

Hakuna mtu aliye salama hadi kila mtu awe salama. Jilinde wewe na jamii yako na upate chanjo ya COVID-19.

Chagua uzima. Pata chanjo ili uepuke kuwa mgonjwa sana kutokana na ugonjwa wa COVID-19!

Kushughulikia Suala la Uoga wa Sindano

“Kudungwa sindano” haraka ni bora kuliko kuwa mgonjwa sana kutokana na ugonjwa wa COVID-19. Hakikisha umechanjwa haraka iwezekanavyo.

Imani na Usalama

Swali: Je, chanjo ya COVID-19 inaweza kuwa na athari za kudumu? Jibu: Chanjo za COVID-19 zinaweza kusababisha athari za muda mfupi kama vile kuhisi uchungu kwenye mkono mahali ulipodungwa sindano au kuchoka/kuongezeka kwa kiwango cha joto mwilini kiasi. Hata hivyo, ni nadra sana kupata athari kali za chanjo.

Swali: Je, chanjo ni salama kwa wanawake wajawazito? Jibu: Chanjo ni salama kwa wanawake wajawazito au wale ambao wangependa kupata ujauzito. Jilinde na upate chanjo ya C-19!

Swali: Je, chanjo za COVID-19 zinasaidia? Jibu: Chanjo zote za COVID-19 zilizoidhinishwa zimethibitishwa kuwa zinasaidia kuzuia watu kutokuwa wagonjwa sana au kufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19. Usingoje! Pata chanjo ya COVID-19 inayopatikana kwanza kwa ajili yako ili ujilinde wewe na wengine.

Swali: Je, chanjo zote za COVID-19 ni salama? Jibu: Chanjo za COVID-19 zinazopatikana katika vituo vya afya vilivyoidhinishwa nchini Kenya zinafanya kazi kama vile tu chanjo za COVID-19 zinazopatikana katika maeneo mengine duniani. Saidia kudumisha afya nchini Kenya na upate chanjo yako haraka iwezekanavyo!

Swali: Je, hatari za COVID-19 ni gani? Jibu: Hatari ya kupata ugonjwa wa COVID-19 inazidi hatari yoyote ya kupata athari kutokana na chanjo ya COVID-19.

Swali: Baada ya kupata chanjo yangu, je, ninaweza kuacha kuvaa barakoa au kuosha mikono? Jibu: Ili kuzuia kupata ugonjwa mkali, pata dozi zote za chanjo ya kujilinda kutokana na ugonjwa wa COVID-19. Hata kama umewahi kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19 hapo awali.

Kushughulikia Suala la Habari za Uongo (Imani na Usalama) - Kuonyesha Dhana Zisizo za Kweli Kuhusu Chanjo ya COVID-19

Si kweli: Chanjo za COVID-19 zinaweza kusababisha utasa kwa wanaume na wanawake. Kweli: Ushahidi hauthibitishi dhana hii. Chanjo za COVID-19 zinaweza kuokoa maisha yako na kufanya uishi miaka mingi ya kupata watoto.

Si kweli: Chanjo za COVID-19 zinaweza kusababisha utasa kwa wanawake. Kweli: Mizunguko ya hedhi ya wanawake wengine hubadilika baada ya kupata kila dozi ya chanjo ya COVID-19, lakini hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa chanjo huathiri ujauzito au uwezo wa kupata ujauzito.

Si kweli: Chanjo za COVID-19 zinaweza kuathiri uwezo wa kuzalisha wa mwanaume. Kweli: Hakuna ushahidi unaothibitisha kwamba chanjo za COVID-19 zinaathiri uwezo wa kuzalisha au kupata ujauzito. Jilinde na upate chanjo ya COVID-19!

Si kweli: Chanjo za COVID-19 husababisha kifo. Kweli: Chanjo za COVID-19 hupunguza zaidi uwezekano wa kulazwa hospitalini au kufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19. Ni nadra sana kupata athari kali za chanjo. Chanjo za COVID-19 zinaokoa maisha.

Si kweli: Ukichanjwa, utapata ugonjwa wa COVID-19. Kweli: Chanjo za COVID-19 hupunguza zaidi uwezekano wa kulazwa hospitalini au kufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19. Ni nadra sana kupata athari kali za chanjo. Chanjo za COVID-19 zinaokoa maisha.

Si kweli: Chanjo za COVID-19 husababisha kifo. Kweli: Kuna uwezekano zaidi wa mtu kufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19 ikiwa hajapata chanjo ya COVID-19 kuliko ikiwa amepata chanjo. Chanjo za COVID-19 zinaokoa maisha.

Viongozi wa Imani

Viongozi wa kidini na jamii huhimiza wanajamii kupata chanjo ya COVID-19 ili kulinda afya yao.

Upatikanaji

Je, unajua kwamba chanjo ya nyongeza ya COVID-19 sasa inapatikana nchini Kenya? Pata chanjo ya nyongeza ili upate ulinzi wa ziada kutokana na ugonjwa wa COVID-19 pindi unapotimiza masharti.

Je, unajua kwamba chanjo za COVID-19 ni za *bure*? Jilinde wewe na wengine na upate chanjo!

Kanuni na Vizuizi vya Kijinsia

Tunapata chanjo ili kudumisha uthabiti na afya ya jamii yetu! [picha inayohusiana ya wanaume]

Saidia wanawake katika jamii yako/Wanawake katika jamii yako wanaweza kuwa na uwezo mdogo wa kupata chanjo ya COVID-19 kuliko wanaume nchini Kenya kwa sababu ya uwezo mdogo wa kusafiri na kufikia vituo vya afya. Mifumo ya afya na watetezi wa wagonjwa lazima wahakikishe kuwa wanawake wana habari na uwezo wanaohitaji ili kupata chanjo.

Kila mtu ana haki ya kupata chanjo za COVID-19. Maafisa wa afya ya umma, makundi ya kutetea wagonjwa na watoa huduma za afya walio katika mstari wa mbele wanaweza kushirikiana ili kuhakikisha kuwa wanawake na watu wenye jinsia mbalimbali wanaweza kupata chanjo za C-19 (Covid-19) na huduma za afya kwa usalama.

Maafisa wa afya ya umma lazima wawasikilize wanawake ili kuelewa njia za kuwafikia ili kuwapa habari za kuaminika kuhusu chanjo za COVID-19. Kuajiri wanawake wa kutoa huduma za chanjo na kuhakikisha mazingira salama na jumuishi ya kazi ni jambo muhimu pia!

Ujumuishwaji wa Walemavu

Watu wenye ulemavu wanaathiriwa na ugonjwa wa COVID-19 kwa njia isiyo sawa. Ni muhimu kuhakikisha uwezo wa kupata habari, huduma na kufikia vituo vya afya katika kukabiliana na COVID-19 nchini.

Habari kuhusu ugonjwa wa COVID-19 na chanjo hazipatikani kila wakati katika miundo ambayo inaweza kufikiwa na watu wenye ulemavu. Hakikisha kuwa watu wenye ulemavu katika jamii yako wana habari wanazohitaji ili kupata chanjo ya COVID-19!

Watu wenye ulemavu huenda wasiwe na uwezo wa kusafiri au kufikia vituo vya afya ili kupata chanjo za COVID-19. Mipango ya kutoa chanjo na viongozi wa jamii lazima wahakikishe kuwa kila mtu anaweza kupata chanjo ya COVID-19!

Graphics

Twitter

Instagram/Facebook

Credits:

Cover photo: CORE Group Polio Project / South Sudan